Friday, 29 August 2025

Kazi na Mchango wa Dkt. Johannes L. Lukumay katika kupigania maendeleo ya jamii

 

Dkt. Johannes L. Lukumay
Mgombea Ubunge - Arumeru Magharibi


Dkt. Johannes Lembulung’ Lukumay alianza taaluma yake ya afya zaidi ya miaka 29 iliyopita akiwa daktari bingwa wa tiba katika vituo vya huduma za afya nchini Tanzania. Baadaye alihudumu kama Mganga Mkuu wa Wilaya (District Medical Officer) katika halmashauri mbalimbali, ambapo alisimamia utoaji huduma za afya, upangaji wa rasilimali, na utekelezaji wa programu za udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

Kupitia uzoefu huo, alijikita zaidi katika uongozi na usimamizi wa afya, akiongoza timu za afya na kushiriki katika kutengeneza mikakati ya kitaifa na ya wilaya. Aliongoza utekelezaji wa sera za afya na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora kwa jamii.

Akiwa Mkuu wa CEDHA (Centre for Educational Development in Health-Arusha), Dkt. Lukumay ameongoza taasisi hiyo katika kubuni na kusimamia programu za mafunzo ya afya kwa ngazi ya diploma na shahada. Amefundisha na kuongoza kozi mbalimbali zikiwemo Leadership and Management, Human Resources Planning and Development, Health Policy and Development, Ethics and Professionalism in Health Services pamoja na mafunzo endelevu (CPD) kama Teaching Methodology and Assessment, Strategic Planning, Basic Hospital Management Training na Policy Analysis.

Aidha, amekuwa mshughulikizi wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi (Public Private Partnership – PPP), na pia msimamizi wa wanafunzi wa diploma katika maandalizi ya tasnifu na tafiti zao.

Dkt. Lukumay pia alifanya kazi kubwa ya kubaini mahitaji ya mafunzo (Training Needs Assessment), kubuni kozi na kuzifundisha katika maeneo ya uongozi, usimamizi wa rasilimali watu, sera za afya, na mbinu za kujifunza na kufundisha kwa walimu wa taasisi za afya nchini Tanzania.

Ujuzi wake wa uongozi na usimamizi uliimarishwa zaidi kupitia mafunzo na warsha ndani na nje ya nchi, zikiwemo Uingereza, Marekani, Uswizi, Ufaransa, Uturuki, Afrika Kusini, Botswana na Lesotho.

Mbali na hayo, Dkt. Lukumay alishiriki kikamilifu katika mradi wa kuadilisha Arusha (Arusha We Want), ambao ulilenga kuibua mawazo, mikakati na sera za kuboresha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Jiji la Arusha. Ushiriki wake katika mradi huo ulihusisha kuchangia mawazo ya kitaalamu kuhusu afya ya jamii, mipango ya rasilimali watu, na uongozi bora wa sekta ya afya, hivyo kuuwezesha mradi huo kuendana na dira ya maendeleo ya afya na elimu.

Katika upande wa utafiti, amejikita katika mifumo ya afya na elimu ya wataalamu wa afya, tathmini ya programu za kujenga uwezo, afya ya uzazi, Malaria, VVU/UKIMWI na magonjwa ya zinaa (STIs).


OKTOBA 29 TUNATIKI #CHAGUA DKT LUKUMAY KWA MAENDELEO


Kazi na Mchango wa Dkt. Johannes L. Lukumay katika kupigania maendeleo ya jamii

  Dkt. Johannes L. Lukumay Mgombea Ubunge - Arumeru Magharibi Dkt. Johannes Lembulung’ Lukumay alianza taaluma yake ya afya zaidi ya miaka ...