Monday, 28 October 2019

KINGA YA MWILI NA VYAKULA

VIJUE VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUONGEZA KINGA YA MWILI

Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya ghafla. Suala la kula pengine ndilo nguzo ya kwanza ya afya ya binadamu Mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote, na usipokuwa sawa basi hutaweza kutimiza lengo lako lolote!

Hivi ni yakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako

*Yogurt (yogati)*
Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza Kinga ya mwili wako

 *PARACHICHI*:
Ukilinganisha na matunda mengine, tunda hili lina virutubisho vingi zaidi na hutakiwi kulikosa kwenye mlo wako kila siku kwani lina virutubisho vifuatavyo: Vitamini K ambayo inaweza kuchangia asilimia 36 ya mahitaji yako mwilini, asilimia 30 ya mahitaji yako ya siku ya vitamini B.
Muhimu zaidi ni kwamba parachichi ni moja ya matunda machache ambayo yana kiasi kikubwa cha mafuta mazuri (god fats) hivyo kupunguza hatari ya kuugua magonjwa ya moyo na uzito mkubwa.

*Vitunguu saumu*:
Hupatikana Kila soko Tanzania! Japokuwa vitunguu saumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali toka enzi za mababu, wataalamu wameshauri pia vitunguu hivi ni chanzo muhimu kwa kinga ya binadamu. Vitumie kwa kutafuna (kama unaweza) au weka kwenye chakula!

*Uyoga*:
Usishangae! Ndio.. hiki ni moja ya vyakula muhimu zaidi kuimarisha afya yako kwani huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!

*Supu ya kuku*
Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto  husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla!

*Viazi vitamu(mbatata)*
Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu.

*Karoti*
Karoti zina ziada kubwa ya vitamin pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti kama kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi!

*Samaki*
Husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa nk.

*Matikiti*

Wengi Hudharau lakini tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilin, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu

*TANGO*
Ni moja ya tunda na mboga inayozalishwa kwa wingi zaidi duniani. Kuweza kutumia tango unaweza kukatakata na ukachanganya kwenye kachumbari yako, ama unaweza kutengeneza juisi kwa kutumia blenda yako ukiwa nyumbani.
Asilimia 90 ya tango ni maji ambapo vifuatavyo ni virutubisho vinavyopatikana: Vitamini K kwa ajili ya kuzuia maambukizi, Vitamini C kwa ajili ya kupambana na maambukizi, vitamini B ambayo huzalisha nguvu kwenye mwili na madini ya manganese kwa ajili ya kuimarisha mifupa.
Kwenye tango kuna madini ya potassium na magnesium kwa ajili ya afya ya moyo pia lina kemikali inayoitwa lignans ambayo hupatikana pia kwenye kabeji na vitunguu ambayo kazi ya lignans ni kupunguza hatari ya kuugua magonjwa ya moyo, pia muungano wa lignin na bakteria wazuri walioko kwenye mfumo wa usagaji chakula husaidia kupunguza hatari ya kuugua badhi ya saratani kama saratani ya matiti, kizazi, na saratani ya tezi dume.

*Maji*
Kama kuna Kitu cha kwanza kwa uhai wa binadamu basi ni maji. Bila kunywa maji ya kutosha bado utakuwa katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali. Angalau lita moja na nusu hadi lita tatu kwa siku ni muhimu kwa afya yako!.

NB: TUMIA CHAKULA KAMA DAWA NA USITUMIE DAWA KAMA CHAKULA

Usisahau ku comment na ku share

No comments:

Post a Comment

Kazi na Mchango wa Dkt. Johannes L. Lukumay katika kupigania maendeleo ya jamii

  Dkt. Johannes L. Lukumay Mgombea Ubunge - Arumeru Magharibi Dkt. Johannes Lembulung’ Lukumay alianza taaluma yake ya afya zaidi ya miaka ...